Wednesday, September 19, 2012

Namanga Sports Club kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka Oktoba 14

Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka
Klabu ya Michezo ya Namanga 'Namanga Sports Club' inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Mwaka, hivyo wanachama wote wanaombwa kuwasilisha michango yao mapema klabuni Leecar's Pub, ili kuweza kufanikisha mkutano huo.

Mkutano Mkuu huo utafanyika Ndege Beach Resort Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Oktoba 14, 2012.

Kwa mawasiliano zaidi waweza piga namba hizi: 0715575712 na 0713605777

Tuesday, May 29, 2012

Namanga Sports Club: Baada ya Mazoezi ni Kujipongeza

Siku ya Jumapili Mei 27. 2012 Klabu ya Michezo ya Namanga ilishiriki katika mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole 'jogging' zilizofanyika huko Kawe jijini Dar es Salaam ambapo vilabu mbalimbali vya jogging vilishiriki. PICHANI: Sehemu ya Wananamanga Sports Club wakijipongeza katika makao Makuu ya Klabu hiyo, yaliyopo Leecar's Pub Barabara ya Kimweri eneo la Msasani Makangira jijini.Picha/John Badi

Mjomba Hafidh akijifua kwa sebene lililokuwa likiporomoshwa klabuni hapo.

Vare naye akisebeneka.

Tuesday, May 8, 2012

MAKTABA YETU

Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka (aliyesimama kushoto), akitoa nasaha kwa wanachama wa klabu hiyo wakati wa tafrija ya mkesha wa mwaka mpya 2009-2010 iliyofanyika katika Makao Makuu ya Klabu yaliyopo Leecar's Pub Barabara ya Kimweri eneo la Msasani - Makangila jijini Dar es Salaam. PICHA/JOHN BADI

Ilipogonga Saa Sita Kamili Usiku mambo yalikuwa hivi.

KUTOKA MAKTABA YETU

Wana -Namanga Sports Club hapa ilikuwa punde baada ya Mkutano Mkuu wa Mwaka ulioenda sambamba na Uchaguzi, uliofanyika katika ukumbi wa Dege Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Aprili 12.2009.

Wana Namanga Sports Club Weekend wanapatikana Leecar's Pub


Wanachama wa Namanga Sports Club siku za weekend  si wazurulaji hupendelea kujipumzisha katika Makao Makuu ya Klabu yao yaliyopo Leecar's Pub,  Barabara ya Kimweri eneo la Msasani Makangila jijini Dar es Salaam.

Wednesday, April 25, 2012

EXTRA BONGO WAFANYA KUFURU MEEDA SINZA JIJINI DAR

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho la kila jumamosi katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.

Mwimbaji Redo Mauzo akiimba wakati wa shoo hiyo.

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho la kila jumamosi katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.

 Mwalimu wa walimu, Banza Stone akiwa kazini.

Hoseah Bass akilichalaza gitaa lake.

Monday, March 26, 2012

Wanamichezo wa Klabu za Michezo za Namanga, Biafra, Kunduchi Kwanza na Kawe wapimwa Afya

Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka akiongoza mamia ya wanamichezo katika kutoa damu ili kupimwa Saratani ya Tezi Dume wakati Kituo cha Kukuza Haki za Binadamu (CHRP), kilipotoa elimu na vipimo bure kwa wanamichezo wa Klabu hiyo na klabu za Biafra, Kunduchi Kwanza na Kawe ikiwa ni katika muendelezo wa Kampeni ya Tanzania 50 Plus. Anayemtoa damu ni Mwanasayansi wa Dawa za Tiba, Daniel Ligola kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS).

Makamu Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Olestick Lembo 'Mjomba Ole' akishiriki zoezi hilo.

Mhazini wa Namanga Sports Club, Michael Juma 'Mo-Power' akishiriki zoezi hilo.

Mdau wa Namanga

Mshauri wa Masuala ya Habari na Mawasiliano wa Namanga Sports Club, John Badi  akishiriki zoezi hilo.

Mjomba akiisikilizia sindano.....

Mdau 'Magoma Moto' naye alishiriki.

Mwenyekiti David Mwaka akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa mtaalamu.

Mzee wa Samaki samaki naye alishiriki.