Friday, December 21, 2012

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Namanga Sports Club wafanyika jijini Dar

Mwanachama wa Klabu ya Namanga Sports, Madeni akiwaimbisha wanachama wa klabu hiyo waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Ndege Beach Resort eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam Desemba 16.2012. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Wageni waalikwa kutoka Klabu ya Biafra Sports.

Kabla ya mkutano kuanza wana-namanga walipasha kidogo ufukweni mwa bahari, wakioongozwa na Mtunza Hazina wa Klabu hiyo, Mike Boss (kulia).

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka (kulia) akijadiliana jambo na Mtunza Hazina wake, Mike Boss. Kushoto nyuma ni Mwanachama Muasisi wa Namanga Sports Club, Bipin Vishan.

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Klabu, Mangole.

Vyeti ya Shukurani na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wale wote walioweza kufanikisha mkutano huo. Aliyetoa zawadi hizo alikuwa ni Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Clement Sanga.


Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka akimkabidhi cheti cha shukrani Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Clement Sanga, ambaye pia kampuni yake iliudhamini mkutano huo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwakaakiangalia Kinyago cha Konyagi kilichotolewa zawadi na klabu kwa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd  ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa mkutano huo kupitia kinywaji chake cha Konyagi.

Mwanachama wa namanga, Kessy Uchungu akipokea kinyago hicho kwa niaba ya kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd.

Wageni waalikwa kutoka Temeke Sports Club.

Mwanachama Bora wa Namanga Sports Club aliibuka kidedea John Gako na cheti chake kilipokelewa na mkewe kutokana na mwenyewe kuwa na udhuru.



Mwananchama wa Namanga, Nunu Sagaf akitoa ufafanuzi kwa wanachama kuhusu uwekezaji wa vipande.

Katibu Mkuu wa Biafra Sports Club, Yahaya Pori (kushoto), akifurahia jambo na Mwanachama wa Namanga,  Mangushi 'Dalia'.


Muda wa maakuli uliwadia.




4 comments:

  1. wenzangu tutembelee web site yetu yapo mara moja moja tupo kibao lakini no comments since 2012. namanga, family family moja wake up. david mwaka

    ReplyDelete
  2. hiyo ndio namanga ya ukweli , sasa tumeyumba kama man u,

    ReplyDelete
  3. mwaka, michael,andrew, ole hafidhi,stiven, gako'bipin,kp,chinga, dulla,henry,na wadau wote wa nguvu mko wapi?

    ReplyDelete
  4. mzee badi hupo sijakuona ,hata wewe mwenye fani yako?

    ReplyDelete