Wednesday, October 17, 2012

Namanga Sports Club yapata Pigo

Marehemu Mkumbo (kushoto), enzi za uhai wake akiwa na viongozi wa Namanga Sports Club wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliofanyika Machi 27.2010 katika Ukumbi wa Ndege Beach nje kidogo ya Jiji la Dar. PICHA/JOHN BADI

Klabu ya Namanga Sports Club imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na Mwanachama wake, Mosses Mkumbo Ndolla aliyefariki dunia katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam Jumapili Oktoba  14,2012 alikokuwa amelazwa.

Mwili wa marehemu Mkumbo uliagwa jana Oktoba 16,2012 baada ya Ibada Maalum iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Msasani na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Iramba Mkoani Singida kwa maziko.

Namanga Sports Club itamkumbuka daima Mpendwa marehemu Mkumbo, kwani pengo aliloliacha haliwezi kuzibika kamwe, hasa kwa ucheshi wake, ukarimu na moyo wa ushirikiano aliokuwa nao.

Namanga Family tulikupenda, lakini Mwenyezi Mungu amekupenda Zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MKUMBO MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

No comments:

Post a Comment