Mwanachama wa Namanga Jogging & Sports Club, Ndugu John Hans Badi ambaye pia ni Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Daily Mitikasi Blog, anachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza hadi maziko ya mpendwa Mama yake Mzazi, Esther Nyimbo Badi (pichani) aliyefariki dunia siku ya Jumatano Feb. 22, 2012 Majira ya Saa 12:30 jioni katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam na baadaye kuzikwa Kijijini Ilembula (W) Njombe, Iringa.
Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari wa Hospitali za Taifa Muhimbili na Aga Khan ambao walikuwa wakipigania ili kuokoa maisha ya mpendwa marehemu Mama yetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.
Shukrani pia ziwaendee Familia yote ya Marehemu Dr. Luhangano Joseph Badi ikiongozwa na Dada yetu Mkubwa Mama Blandina Nyoni, shemeji zetu kwa jitihada walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Mama yetu.
Pia nawashukuru Wanahabari, Wana Namanga Family, Bloggers na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijumuika nami katika kunifariji na kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu, ama kwa njia ya simu, E-mails au ana kwa ana.
Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja ila shukrani pia ziwaendee Askofu Alex Malasusa, Askofu Owdenburg Mdegela, Askofu Mengele, Wachungaji, Uongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa, Mbunge wa Njombe Magharibi, Gerson Lwenge, Naibu Waziri Wa Afya, Dr. Lucy Nkya, Mama Mdogo Eliza, Binamu zetu , wana Ilembula, Wakazi wa Wilolesi Iringa pamoja ndugu jamaa na marafiki.
Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (Mama Esther Nyimbo Badi) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!
Mungu ampumzishe Mama Esther Nyimbo Badi Mahala Pema Peponi – Amen!

No comments:
Post a Comment