Sunday, January 4, 2015

NAMANGA SPORTS CLUB YAUKARIBISHA MWAKA MPYA KWA SHANGWE



Mwakilishi wa Klabu ya Biafra Sports, akitoa nasaha zake wakati wa tafrija ya mkesha kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka 2015, iliyoandaliwa na Klabu ya Namanga Sports katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam Desemba 31. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga Sports, Olestick Lembo. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Baadhi ya viongozi wa Klabu ya Biafra Sports na Klabu ya Namanga Sports, wakitosti kama ishara ya kuukaribisha mwaka mpya.


Mlezi wa Namanga Sports Club, Mzee Juma (katikati), akisoma dua la kuukaribisha mwaka mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga Sports, Olestick Lembo na Mwenyekiti wa Biafra Sports, Bwana Mollel.

Thursday, April 11, 2013

Namanga Sports Club yashiriki uzinduzi wa Klabu ya Msasani Jogging

Msasani Jogging wakiongoza Jogging.


Mgeni rasmi Phares Magesa akiwahutubia wanamichezo. Kulia anayechati na simu ni Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka.
Klabbu ya Namanga Sports ilishiriki katika Uzunduzi wa Klabu ya Msasani Jogging uliofanyika Jumapili Aprili 07. 2013 katika Ufukwe wa Msasani jijini Dar es Salaam.

Katika hafla ya uzinduzi huo Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Shrikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Bw. Phares Magesa.

Zaidi ya  wanamichezo 800 kutoka zaidi ya Klabu 20 vya Jogging walihudhuria akiwemo Diwani wa Kata ya Msasani (CCM), Mheshimiwa Christina Kirigiti.

Baadhi ya klabu zilizoshiriki uzinduzi huo ni pamoja Biafra, Kunduchi Kwanza, Msufini, Family Jogging, Kawe Social & Sports Club, Kawe Beach Jogging na Kunduchi Kwanza.

Klabu zingine ni pamoja na Sotojo, Ukwamani Jogging, Barafu, Mzimuni, Kata 14, Kongowe, Timberland,Unga Unga Jogging, Fanja Jogging, Dovya Jogging n.k. Habari picha kwa hisani ya Biafra Blog

Friday, March 15, 2013

KIKAO CHA HARUSI YA JAMAL JOHN GAKO

Kikao cha tatu cha Harusi ya Mwanachama wa Namanga Sports Club, John Gako a.k.a JAMAL (pichani), kinatafanyika Jumapili Machi 17, 2013 katika Leecar's Pub iliyoko katika eneo la Namanga - Msasani Makangila barabara ya Kimweri jijini Dar es Salaam.

Wanamichezo toka klabu za Kunduchi Kwanza, Biafra, Namanga na vilabu vingine rafiki, wadau, wote, ndugu, jamaa na marafiki wanaombwa kuhudhuria kwa wingi ili tuweze kufanikisha Harusi ya mwanamichezo mwenzetu.

Gako anatarajia kufunga ndoa Mwishoni mwa Mwezi April.

NB: Mkija na michango ni bora zaidi, kwani muda uliobaki ni mdogo sana.

Imetolewa na:
John Badi
Mshauri wa Masuala ya Habari na Mawasiliano
Namanga Sports Club

Namanga Sports Club yashiriki mazoezi na Harambee ya Kunduchi Kwanza

Mnamo Machi 10, 2013 wanamichezo kutoka Namanga Sports Club, Kawe Beach, Kawe Social & Sports Club, Msasani Jogging & Sports Club, Biafra Sports Club pamoja na wenyeji Kunduchi Kwanza walikusanyika pamoja na kufanya mazoezi ya Jogging ambapo zaidi ya wanamichezo 100 walikutana pamoja na wadau wengine. Mbio hizo zilianzia Makao Makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza Malanja Pub iliyopo Kunduchi Mtongani kupitia Mbuyuni, Afrikana hadi round about ya Kawe na kisha kurudia njia hiyo hiyo hadi Malanja. PICHANI: Mweka Hazina wa Namanga, Michael Juma 'Mike Boss' (katikati mstari wa mbele) akiongoza mazoezi ya viungo (Aerobics). Picha kwa hisani ya Biafra Blog

Sehemu ya wakimbiaji.

Wana-Namanga pia walishiriki harambee.

Makamu Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Uncle Ole (kulia) na Mweka Hazina, Mike Boss wakitafakali jambo wakati wa harambee hiyo.

Friday, December 21, 2012

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Namanga Sports Club wafanyika jijini Dar

Mwanachama wa Klabu ya Namanga Sports, Madeni akiwaimbisha wanachama wa klabu hiyo waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Ndege Beach Resort eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam Desemba 16.2012. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Wageni waalikwa kutoka Klabu ya Biafra Sports.

Kabla ya mkutano kuanza wana-namanga walipasha kidogo ufukweni mwa bahari, wakioongozwa na Mtunza Hazina wa Klabu hiyo, Mike Boss (kulia).

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka (kulia) akijadiliana jambo na Mtunza Hazina wake, Mike Boss. Kushoto nyuma ni Mwanachama Muasisi wa Namanga Sports Club, Bipin Vishan.

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Klabu, Mangole.

Vyeti ya Shukurani na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wale wote walioweza kufanikisha mkutano huo. Aliyetoa zawadi hizo alikuwa ni Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Clement Sanga.


Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwaka akimkabidhi cheti cha shukrani Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Clement Sanga, ambaye pia kampuni yake iliudhamini mkutano huo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Namanga, David Mwakaakiangalia Kinyago cha Konyagi kilichotolewa zawadi na klabu kwa kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd  ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa mkutano huo kupitia kinywaji chake cha Konyagi.

Mwanachama wa namanga, Kessy Uchungu akipokea kinyago hicho kwa niaba ya kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd.

Wageni waalikwa kutoka Temeke Sports Club.

Mwanachama Bora wa Namanga Sports Club aliibuka kidedea John Gako na cheti chake kilipokelewa na mkewe kutokana na mwenyewe kuwa na udhuru.



Mwananchama wa Namanga, Nunu Sagaf akitoa ufafanuzi kwa wanachama kuhusu uwekezaji wa vipande.

Katibu Mkuu wa Biafra Sports Club, Yahaya Pori (kushoto), akifurahia jambo na Mwanachama wa Namanga,  Mangushi 'Dalia'.


Muda wa maakuli uliwadia.




Friday, November 23, 2012

MKUTANO MKUU WA NAMANGA SPORTS CLUB KUFANYIKA DESEMBA 09 NDEGE BEACH



Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, David Mwaka akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu, kilichofanyika Leecar's Pub Namanga jijini Dar es Salaam jana jioni. PICHA/JOHN BADI
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na John Badi
 
Mkutano Mkuu Maalum wa Klabu ya Namanga Sports unatarajiwa kufanyika Desemba 09, mwaka huu katika Ukumbi wa Ndege Beach uliopo katika eneo la Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi, Mwenyekiti wa Namanga Sports Club, Bw. David Mwaka alisema tayari makampuni kadhaa yameshajitokeza kudhamini mkutano huo.

Bw. Mwaka aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Tanzania Distilleries Ltd watengenezaji wa kinywaji maarufu cha Konyagi, Mike Commercial, Esoshi General Trading Co. Ltd na Mele DJ Co. Ltd ya Dodoma.

"Tunawashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha onyesha moyo wa kutusaidia, lakini pia tunawaomba wadhamini wengine wajitokeze zaidi ili tuweze kufanikisha mkutano wetu", alisema Bw. Mwaka.

Aidha Bw. Mwaka alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo ambao bado hawajatoa michango yao ya 20,000/- kuiwasilisha mara moja kwa watu waliopewa majukumu ya kukusanya ambao ni John Gako, Bebee Mangi na Chale JJ.

Pia wanachama wote wanatakiwa kuhudhuria kikao kingine kitakachofanyika Jumapili Desema 25, pale Leecar's Pub Namanga.

Wednesday, October 17, 2012

Namanga Sports Club yapata Pigo

Marehemu Mkumbo (kushoto), enzi za uhai wake akiwa na viongozi wa Namanga Sports Club wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliofanyika Machi 27.2010 katika Ukumbi wa Ndege Beach nje kidogo ya Jiji la Dar. PICHA/JOHN BADI

Klabu ya Namanga Sports Club imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na Mwanachama wake, Mosses Mkumbo Ndolla aliyefariki dunia katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam Jumapili Oktoba  14,2012 alikokuwa amelazwa.

Mwili wa marehemu Mkumbo uliagwa jana Oktoba 16,2012 baada ya Ibada Maalum iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Msasani na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Iramba Mkoani Singida kwa maziko.

Namanga Sports Club itamkumbuka daima Mpendwa marehemu Mkumbo, kwani pengo aliloliacha haliwezi kuzibika kamwe, hasa kwa ucheshi wake, ukarimu na moyo wa ushirikiano aliokuwa nao.

Namanga Family tulikupenda, lakini Mwenyezi Mungu amekupenda Zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MKUMBO MAHALA PEMA PEPONI AMEN.